Ajali Morogoro: Wanne wafariki na 21 kujeruhiwa
Watu
wanne wamefariki dunia leo na wengine 21 kujeruhiwa kufuatia basi
aina ya Isuzu kugonga treni ya abiria iliyokuwa ikienda bara katika
kilomita 276/0 kati ya stesheni za Kimamba na Kilosa Mkoani Morogoro
wilayani Kilosa majira ya saa 11:25 asubuhi ya leo.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotoewa na ofisi ya Uhusiano kwa niaba ya Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Elia Mshana amesema basi hilo lenye
namba za usajili T 837 CTM Isuzu Coaster linalomilikiwa na Feisal A.
Khuwel wa Kilosa.
Taarifa
kutoka eneo la tukio limefafanua kuwa waliofariki ni wanaume wawili,
mwanamke mmoja na mtoto wa miaka minne. Kwa upande wa majeruhi, majeruhi
21 wako wanaume 14 na wanawake 7 ambao wanaendelea na matibabu katika
Hospital ya Wilaya ya Kilosa.
Hata
hivyo baada ya ajali treni ya abiria imeondoka katika stesheni ya
Kilosa saa 3 asubuhi kuendelea na safari yake kwenda Bara.


Comments
Post a Comment