simba yasaka makocha wa viungo

SIMBA jeuri! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya klabu hiyo kumalizana na kocha kutoka Uingereza pamoja na wasaidizi wake wawili kutoka nchini humo ambao wote watatua nchini muda wowote kuanzia sasa.
Simba imeona ni vema kuajiri makocha wenye kila aina ya ujuzi unaotakiwa katika klabu ya soka, akiwamo mtaalamu wa mazoezi ya viungo, ya uwanjani ya mambo ya mbinu na ufundi ambayo yatasimamiwa na kocha mkuu.
Habari za ndani kutoka Simba zinasema tayari wamefanikiwa kuwapata makocha hao watatu ambao majina yao yatafahamika siku chache kabla ya kutua nchini tayari kuleta changamoto mpya ndani ya kikosi chao msimu ujao.

Comments

Popular posts from this blog

Pichaz za matukio yaliyo jiri magufuli alipokuwa chato leo

Crystal Palace kuivaa Man united –FA CUP