Simba Yafikia Uamuzi Wa Kumpeleka Singano Polisi

pichani ni haji mannara msemaji wa( simba sc)
UONGOZI wa Simba umesema umeamua kulifikisha polisi sakata la usajili wa kiungo mshambuliaji Ramadhani Singano ‘Messi’ ili kulinda taswira ya klabu hiyo.
Messi anadai kutotambua uhalali wa mkataba wake wa miaka mitatu na Simba uliopo katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) huku akisisitiza ana mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo ya Msimbazi utakaomalizika Julai Mosi mwaka huu
Hajji Manara msemaji wa Simba katika mahojiano na moja ya vituo vya redio leo amesema kuwakuwa kutokana na mvutano ulioibuka baina ya pande zote mbili, klabu imeona ni vyema kulifikisha suala hilo mbele ya vyombo vya dola ili lipatiwe ufumbuzi.
“Simba ni taasisi kubwa, suala hili linachafua ‘image’ (taswira) ya taasisi hii. Tukumbuke pia kwamba Simba ina wadhamini. Inaposemwa kwamba tumeghushi nyaraka likiwamo dole gumba la Messi ni kashfa kubwa. Wadhamini wanatuelewaje?” Amehoji Manara bila kutaja lini hasa suala hilo litatinga polisi
Wakati Simba wakitishia kulifikisha suala hilo mikononi mwa polisi tayari Chama cha Wachezaji wa Soka Tanzania (Sputanza) kimeshalifikisha sakata hilo mikononi mwa TFF ili litatuliwe na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya shirikisho hilo
Mwenyekiti wa Sputanza Mussa Kisoky alisema jijini jana kuwa walifikia hatua ya kuonana na uongozi wa TFF baada ya kupewa maelezo na winga huyo mwenye umri wa miaka 21.
Comments
Post a Comment