IDADI YA WATU WALIOFARIKI KATIKA AJALI ZA BARABARANI HIVI KARIBUNI
Jumla ya watu 103 wamepoteza maisha katika matukio makubwa ya ajali yaliyotokea kwa kipindi cha mwezi mmoja katika maeneo mbalimbali hapa nchini huku idadi ya majeruhi katika ajali hizo ikifikia watu 138 na baadhi ya majeruhi wakibaki na ulemavu wa kudumu.
Watu 103 kupoteza maisha na watu 138 kujeruhiwa ikiwemo wengine
kupata ulemavu wa kudumu imetokea kwa kipindi cha mwezi mmoja tu katika
maeneo mbalimbali hapa nchini,huku chanzo kikubwa cha ajali hizi
zilizopoteza maisha ya watanzania imedaiwa kusababishwa na uzembe wa
baadhi ya madereva.
Jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani mbali na kubaini
vyanzo vya ajali hizo zilizotokea katika maeneo mbalimbali nchini kwa
kutaja kuwa ni uzembe wa baadhi ya madereva,tatizo la mwendo kasi,ubabe
wa baadhi ya madereva kwa magari madogo,mkuu wa kikosi cha usalama
barabarani Mohamed Mpinga,amelazimika kuweka wazi idadi ya vifo
vilivyotokea katika ajali mbalimbali kuanzia mwezi january mwaka
huu,ambapo watu wengi wamepoteza maisha.
Baadhi ya wanasheria wamesema kuna udhaifu mkubwa katika sheria
inayotumika,kwani licha ya madereva na wamiliki wa mabasi na magari
binafsi wakugundulika kusababisha watu kupoteza maisha kutokana na
uzembe wao,hakuna sheria kali inayotumika kuwabana mbali na kutozwa
faini ndogondogo huku ndugu wa marehemu waliopoteza maisha katika ajali
hizo pamoja na majeruhi hasa wale waliachwa na ulemavu wa kudumu
wakibaki njia panda bila kupewa fidia yeyote na wamiliki wa vyombo
hivyo.
ITV
Comments
Post a Comment