Ratiba ya kufuzu mashindano ya 4 ya CHAN

CAF itapanga ratiba ya CHAN 2016, Aprili 5.
Ratiba ya kufuzu mashindano ya 4 ya CHAN yatakayofanyika nchini Rwanda mwaka 2016 itafanyika Jumapili, Aprili 5, 2015 katika Makao Makuu ya CAF jijini Cairo, Misri.
Mataifa 42 yanatarajiwa kushiriki katika kuwania kupata tiketi 15 za kushiriki michuano hiyo mahususi kwa ajili ya wachezaji wanaocheza ligi za ndani ya mipaka ya nchi zao.
Timu hizo 42 zitagawanywa kulingana na kanda za Kisoka barani Afrika.
Timu na kanda ni kama ifuatavyo:
* Kanda ya Kaskazini ( Nafasi 2) - Libya, Morocco, Tunisia
* Kanda ya Magharibi A (Nafasi 2) - Gambia, Guinea, Guinea Bissau, Liberia, Mali, Mauritania, Senegal, Sierra Leone
* Kanda ya Magharibi B (Nafasi 3) - Burkina Faso, Ivory Coast, Ghana, Niger, Nigeria, Togo
*kanda ya kati ( Nafasi 3) - Cameroon, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Congo, Chad, DR Congo, Gabon
*Kanda ya Afrika Mashariki (Nafasi 3 skiwemo mwenyeji Rwanda ) - Burundi, Djibouti, Ethiopia, Kenya, Sudan, Tanzania, Uganda
* Kanda ya Kusini (3 matangazo) - Angola, Botswana, Comoro, Mauritius, Lesotho, Msumbiji, Namibia, Shelisheli, Afrika Kusini, Swaziland, Zambia, Zimbabwe
Kutakuwa na hatua mbili za kufuzu kwa kila kanda isipokuwa kwa Kanda ya Kaskazini, ambapo timu tatu zitacheza kwa mtindo wa makundi na mbili za juu zitafuzu.
Mechi za kufuzu zitachezwa mwishoni mwa wiki ya 19-21 Juni mwaka 2015 huku marudiano yakipigwa kati ya tarehe 28-30 Agosti 2015 ambapo timu 15 zitajiunga na mwenyeji Rwanda kwa ajili ya fainali za CHAN zitakazoanza Januari 16 -Februari 7 2016.
Washindi wa Mashindano ya CHAN yaliyopita ni:DR Congo (2009), Tunisia (2011) na Libya (2014).

Comments

Popular posts from this blog

Pichaz za matukio yaliyo jiri magufuli alipokuwa chato leo

Crystal Palace kuivaa Man united –FA CUP