Maamuzi ya FIFA kwa Zimbabwe kuhusu Michuano ya Kombe la Dunia 2018
Mechi za kufuzu kwa michuano hiyo
kwaupande wa nchi za Afrika zinatarajiwa kuanza mwezi October mwaka
huu, Zimbabwe ni moja ya nchi za Afrika ambazo hazijawahi kufuzu
kucheza mechi za Kombe la Dunia.
Taarifa kutoka FIFA leo inahusu uamuzi
uliotolewa kwamba Zimbabwe imepigwa marufuku kushiriki katika mechi za
kufuzu kombe la dunia kwa mwaka 2018, baada ya kuwepo kwa taarifa za
nchi hiyo kukataa kumlipa kocha wake wa zamani, Jose Claudinei Georgini.
Taarifa iliyotolewa na Shirikisho la
soka Duniani FIFA imesema kuwa, imechukua hatua hiyo baada ya nchi hilo
kushindwa kumlipa kocha huyo na kuongezea kuwa shirikisho la soka
Zimbabwe, ZIFA lilishindwa kulipa deni hilo mbali ya kwamba walipewa
muda wa kutosha ili kufanya malipo hayo.

Comments
Post a Comment