SOMA HAPA MOJA KATI YA HABARI ZA LEO KATIKA GAZETI LA MTANZANIA
Zitto Kabwe ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Mwigulu Nchemba, Mbunge wa Iramba Magharibi na pia Naibu Waziri wa Fedha jana walialikwa kushiriki mahojiano katika kipindi cha Jambo Tanzania
kinachorushwa na Televisheni ya Taifa (TBC) ambapo katika mjadala huo
kila mmoja kumsifia mwenzake kwa utendaji kazi uliotukuka.
Katika mjadala huo, Mwigulu ambaye ni mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliyeanza kummwagia sifa Zitto kwa jinsi ambavyo amekuwa akitekeleza majukumu yake ya kiuongozi katika nafasi yake ya uenyekiti wa Kamati ya PAC.
Mwigulu alisema Zitto
na kamati yake kwa ujumla wamekuwa wakifanya kazi kubwa na nzuri ya
kibunge na pia kuishauri vizuri serikali na hasa Wizara ya Fedha.
Zitto alijibu pongezi hizo muda mfupi kabla ya kuhitimishwa kwa mjadala huo kwa kueleza kuwa iwapo Mwigulu
ataonyesha nia ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa baadaye mwaka
huu atamuunga mkono, kwa sababu ameonyesha kuwa ni kiongozi mzalendo na
mwenye uwezo mkubwa wa kuelewa matatizo ya wananchi na kuyatafutia
ufumbuzi.
Wabunge hao wameonyesha dhamira ya
kuunganisha nguvu zao ili kutekeleza malengo yao ya kisiasa, huku kukiwa
na mitazamo mbalimbali ndani na nje ya jamii kuhusu wanasiasa vijana
waliokwishaonyesha nia ya kuwania madaraka hayo ya juu ya Dola.
Kitengo cha jarida la ‘The Economist’ cha The Intelligence Unit
ambacho hufanya ufuatiliaji wa siasa za kimataifa, mwishoni mwa mwaka
jana kilimtaja Zitto kuwa ni mmoja wa wanasiasa vijana wa kambi ya
upinzani ambaye ana nguvu kkubwa kisiasa.
The Intelligence Unit kilieleza kuwa umaarufu wa kisiasa wA zito
unatokana na nafasi yake ya kiongozi wa kamati nyeti ya Bunge ambayo
imekuwa ikiibua mambo mazito na yenye athari katika taifa, hivyo licha
ya kuwa na mgogoro na baadhi ya viongozi wenzake ndani ya CHADEMA, bado
anao ushawishi mkubwa wa kisiasa kwa wadhifa alionao ndani ya Bunge.
rais
Comments
Post a Comment