chelsea vs liverpool CAPITAL ONE CUP watoka sare bao moja kwa moja
- Details
- Created: Wednesday, 21 January 2015 05:55
Mechi ya kwanza ya Nusu Fainali ya Kombe la Ligi, sasa maarufu kama Capital One Cup, kati ya Liverpool na Chelsea ilimalizika kwa Sare ya 1-1 Uwanjani Anfield Jana Usiku.
Chelsea ndio walikuwa wa kwanza kupata Bao kwa Penati ya Eden Hazard iliyotolewa na Refa Martin Atkinson katika Dakika ya 17 baada ya Emre Can kumuangusha Hazard.
Liverpool walisawazisha kwa Bao la Raheem Sterling kufuatia juhudi zake binafsi katika Dakika ya 59.
Leo itachezwa Nusu Fainali nyingine huko White Hart Lane Jijini London kati ya Tottenham Hotspur na Sheffield United inayocheza Ligi Daraja la chini la Ligi 1 likiwa ni Daraja la 3 toka Ligi Kuu England.
Marudiano ya Nusu Fainali hizi yatafanyika Wiki ijayo ambapo safari hii Mechi zitachezwa Nyumbani kwa Timu zilizokuwa Ugenini.
Comments
Post a Comment