Azam fc waichapa kagera sugar 3 1ligi kuu vodacom

MABINGWA Watetezi wa Ligi Kuu Vodacom Azam FC Leo hii huko Jijini Mwanza wameichapa Kagera Sugar Bao 3-1 na kushika nafasi ya kwanza kwenye Ligi hiyo.
Hadi Mapumziko, Azam FC walikuwa mbele 2-0 ya Wenyejji wao  Kagera Sugar ambao hivi sasa wanatumia CCM Kirumba kama Uwanja wa Nyumbani baada ya Kaitaba huko Bukoba kufungwa kwa ukarabati.
Bao za Azam FC zilifungwa na Kipre Tchetche na Didier Kavumbagu katika Kipindi cha Kwanza na Kipindi cha Pili Kagera Sugar wakapata Bao 1 kupitia Rashid Mandawa lakini ni tena Kavumbagu akawahakikishia ushindi kwa kupiga Bao la 3.
Ushindi huu umewafanya Azam FC kuipiku Mtibwa Sugar na kuongoza Ligi wakiwa Pointi 3 mbele yao lakini Mtibwa Sugar wamecheza Mechi 1 pungufu.
Mechi ijayo kwa Azam FC ni hapo Jumamosi Jijini Dar es Salaam watakapoivaa Simba.

Comments

Popular posts from this blog

Pichaz za matukio yaliyo jiri magufuli alipokuwa chato leo

Crystal Palace kuivaa Man united –FA CUP