Serikali yatangaza siku maalum ya usafi

Serikali imeitangaza rasmi siku ya jumamosi ya kila mwisho wa mwezi kuwa ni siku ya usafi na kwamba hatua za kisheria na kinidhamu zitachukuliwa kwa watendaji wowote watakaoshindwa kutekeleza agizo hilo.
Agizo hilo limetolewa jijini Dar es Salaam na naibu waziri wa ofisi ya makamo wa rais, muungano na mazingira Bw Luoga Mpina ambapo amesema agizo hilo linaanza mara moja huku akisisitiza kuwa lengo kubwa ni kupambana na magonjwa yanaweza kusababishwa na uchafu.
Kuhusu athari za mabadiliko ya tabia nchi waziri Mpina amesema Tanzania hupoteza zaidi ya heka laki nne za misitu kila mwaka huku joto la dunia likiongeza kwa nyuzi joto 0.85, ambapo pia kina cha bahari kikiongeka hadi kufikia 19 cm, pia akatumia fursa hiyo kutoa agizo kwa halimashauri zote nchini.
Kwa mujibu wa taarifa za wizara hiyo ya makamo wa rais muungano na mazingira, Tanzania inazaidi ya hekta milioni 48.1 za misitu ambayo hutumika kumeza hewa ya kabon tirion 9.03 ambapo juhudi za upandaji miti zikitajwa kusaidia kuondoa athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Comments